Sunday 4 January 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO YA CHETI CHA FAMASI



Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Afya Mtwara (MHTI)/ COTC Mtwara anawatangazia wahitimu wa kidato cha Nne/Sita na wananchi wote kuwa taasisi inatarajia kuanza kutoa kozi ya Famasi kwa ngazi ya Cheti (Basic Technician Certificate NTALevel 4 Course in Pharmaceutical Sciences) kuanzia Februari, 2015.  Kozi hii ni ya muda wa mwaka mmoja.

Sifa za mwombaji:
·        Awe amemaliza kidato cha nne.
·        Awe na ufaulu wa masomo matatu yakiwemo mawili ya sayansi Biologia na Kemia katika kiwango cha alama D.
·        Awe na uwezo wa kugharamia gharama za mafunzo.
·        Awe na uwezo wa kuishi maisha ya kujitegemea nje ya chuo.

Jinsi ya kuomba,
·        Fomu za maombi zinapatikana katika Ofisi ya Kanda (Mtwara COTC), Halmashauri za wilaya zote (Lindi na Mtwara) kupitia Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Vyuo vya Afya Kanda ya Kusini (Newala NTC, Nachingwea NTC, Mkomaindo NTC, CATC Masasi, Mtwara NTC, Lindi COTC) Taasisi za Dini (Nyangao hospital, Nyangao School of Nursing, Ndanda school of Nursing, Mnero hospital, Kilwa kipatimu Hospital, na mashirika yasiyo ya serikali, mbao za matangazo, vituo vya afya n.k
·        Gharama ya fomu ni Tshs. 15,000/=. 
·        Malipo yote yalipiwe benki katika akaunti ya Chuo Namba 70610004938, MTWARA MEDICAL TRAINING CENTRE PROJECT, NMB MTWARA BRANCH.
·        Mwombaji anaporudisha fomu ahakikishe ameambatanisha nakala za vyeti vilivyohakikiwa na mwanasheria wa serikali pamoja na risiti halisi ya benki (Original bank pay-in slip).
·        Picha moja ya passport size ya hivi karibuni.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/01/2014

Kwa  mawasiliano zaidi:
Unaweza kuandika barua kwa,
Mkuu wa Chuo,
Taasisi ya Mafunzo ya Afya,
S.L.P 86,
MTWARA.

Namba za simu:  0784-358582/0715-358582 au 0719-676192/0756-683231

No comments:

Post a Comment