Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Afya Mtwara (MHTI)/ COTC Mtwara anawatangazia
wahitimu wa kidato cha Nne/Sita na wananchi wote kuwa taasisi inatarajia kuanza
kutoa kozi ya Famasi kwa ngazi ya Cheti (Basic Technician Certificate NTALevel 4 Course in Pharmaceutical
Sciences) kuanzia
Februari, 2015. Kozi hii ni ya
muda wa mwaka mmoja.
Sifa za
mwombaji:
·
Awe
amemaliza kidato cha nne.
·
Awe
na ufaulu wa masomo matatu yakiwemo mawili ya sayansi Biologia na Kemia katika
kiwango cha alama D.
·
Awe
na uwezo wa kugharamia gharama za mafunzo.
·
Awe
na uwezo wa kuishi maisha ya kujitegemea nje ya chuo.
Jinsi ya kuomba,
·
Fomu
za maombi zinapatikana katika Ofisi ya Kanda (Mtwara COTC), Halmashauri za wilaya zote (Lindi na Mtwara)
kupitia Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Vyuo vya Afya Kanda ya Kusini (Newala
NTC, Nachingwea NTC, Mkomaindo NTC, CATC Masasi, Mtwara NTC, Lindi COTC) Taasisi
za Dini (Nyangao hospital, Nyangao School of Nursing, Ndanda school of Nursing,
Mnero hospital, Kilwa kipatimu Hospital, na mashirika yasiyo ya serikali, mbao
za matangazo, vituo vya afya n.k
·
Gharama
ya fomu ni Tshs. 15,000/=.
·
Malipo
yote yalipiwe benki katika akaunti ya Chuo Namba
70610004938, MTWARA MEDICAL TRAINING CENTRE PROJECT, NMB MTWARA BRANCH.
·
Mwombaji
anaporudisha fomu ahakikishe ameambatanisha nakala za vyeti vilivyohakikiwa na
mwanasheria wa serikali pamoja na risiti halisi ya benki (Original bank pay-in
slip).
·
Picha
moja ya passport size ya hivi karibuni.
Mwisho wa
kupokea maombi ni tarehe 31/01/2014
Kwa
mawasiliano zaidi:
Unaweza kuandika
barua kwa,
Mkuu wa Chuo,
Taasisi ya Mafunzo
ya Afya,
S.L.P 86,
MTWARA.
Namba
za simu: 0784-358582/0715-358582 au
0719-676192/0756-683231
Barua pepe: info_zhtimtwara@yahoo.com
No comments:
Post a Comment